Sungura kabila ya Newzealand White na Chinchilla wakiwa kwenye cage. |
Sungura anaweza kufugwa ima kwa ngazi ya familia au kibiashara na kuwa chanzo bora cha cha nyama, pia sungura anasifa nyingi ukilingalinisha na wanyama wengine wanaofugwa kama kuku, mbuzi, nguruwe, na ng'ombe sifa hizi ni;
1. Sungura anauwezo wa kuzaa watoto wengi kwa kila mzao na mara nyingi kwa mwaka, sungura mmoja anauwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 1 kwa mzao mmoja na kuzaa mara 5 hadi 6 kwa mwaka.
2. Sungura anauwezo mkubwa wa kubadili zaidi ya asilimia 20℅ ya chakula cha protein anachokula kuwa katika hali ya nyama na kuweza kuliwa kama chanzo cha nyama ukilinganisha na asilimia 12℅ ya ng'ombe na 18℅ ya nguruwe.
3. Sungura anaweza kufugwa kwenye eneo dogo la ardhi ukilinganisha na mfugo mwingine wowote, kwani eneo la robo heka unaweza ukafuga sungura hadi 200.
4. Nyama ya sungura ni miongoni mwa nyama nyeupe kama nyama ya samaki na ina ladha nzuri sana ukilinganisha na nyama za mifugo mingine. Pia kiafya inashauriwa kutumia nyama ya sungura kwani ina virutubisho vingi na haina cholesterol.
5. Nyama ya sungura haina makatazo kwa dini na mila nyingi kwa hapa nchini na duniani kote.
6. Sungura hawasumbuliwi sana na magonjwa ukilinganisha na mifugo mingine kama vile kuku, mbuzi, nguruwe na ng'ombe.
7. Sungura hawana ushindani mkubwa wa chakula na binadam ukilinganish mifugo kama kuku na nguruwe kwani wanaweza kufungwa kwa kulishwa majani na kiasi kidogo cha nafaka.
8. Licha ya nyama sungura pia anaweza kukupatia mazao kama mbolea, ngozi na mkojo wake ambao unatumika katika kuuwa na kuteketeza wadudu waharibifu kwenye mazao ya shambani na bustani.
No comments:
Post a Comment