Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu duniani kumesababisha kuongezaka uhitaji wa chakula bora hususani chanzo bora cha nyama. Hivyo basi ufugaji wa sungura ni miongoni ya shughuli inayokuwa kwa kasi sana hapa nchini na duniani kote ili kuweza kuzalisha nyama kwa wingi na kukabiliana na uhitaji huu mkubwa wa nyama kote duniani.
|
Sungura kabila ya Newzealand White na Chinchilla wakiwa kwenye cage. |
Sungura anaweza kufugwa ima kwa ngazi ya familia au kibiashara na kuwa chanzo bora cha cha nyama, pia sungura anasifa nyingi ukilingalinisha na wanyama wengine wanaofugwa kama kuku, mbuzi, nguruwe, na ng'ombe sifa hizi ni;